Jumamosi hii ya Juni 4 mbona ‘kitanuka’ Dar Live! Ni usiku wa nani
mkali kutoka kwa mastaa wa taarab, bongo fleva na singeli.
Ni onyesho kubwa la na mwisho kabla kuelekea mapumziko ya mwezi
mtufu wa Ramadhan ambapo Isha Mashauzi akiwa na kundi zima la
Mashauzi Classic ataumana jukwaa na Snura, Roma Mkatoliki, Sholo
Mwamba na Man Fongo.
Msemaji wa ukumbi wa Dar Live, Juma Mbizo amesema onyesho hilo
la kipekee limezingatia muziki wa kila njanja ili kuleta ladha
isiyochuja mwanzo hadi mwisho wa show.
Mbizo amesema kupitia onyesho hilo mashabiki watajionea wenyewe
ni mzuiki upi wenye nguvu zaidi kati ya taarab, bongo fleva, singeli na
hata rumba kutokana na ukweli kuwa Isha Mashauzi mbali na taarab
lakini pia ana ngoma zake kali za muziki wa rumba.
Naye Isha Mashauzi amesema atalitendea haki onyesho hilo hasa
kutokana na ukweli kuwa hajapanda jukwaa la Dar Live kwa takriban
miaka miwili na hivyo hiyo ni nafasi pekee ya kutaka kiu ya
mashabiki wake watakaofika kwenye ukumbi huo mkubwa zaidi wa
burudani ulioko maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...