Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Boniface Jacob akiwaonesha waandishi wa habari ramani inayoonyesha eneo la makaburi lililovamiwa na taasisi ya Mkapa Foundation ambalo limegaiwa na manispaa kinyume na taratibu. Kwa maelezo ya nyaraka za manispaa zinavyoonyesha, eneo hilo limetolewa wakati baraza la madiwani likiwa limemaliza muda wake. Cha kushangaza eneo hilo, manispaa haijaambulia hata shilingi. Na mwisho kabisa mstahiki meya, ameaagiza kusimamishwa shughuli zozote katika eneo hilo.
Meya wa manispaa ya kinondoni Mhe. Boniface Jacob amepiga marufuku watendaji wa manispaa hiyo kuacha tabia ya kubadirisha hati za viwanja vilivyotengwa kwa ajili ya kuzikia kwenda kwenye ujenzi wa huduma za watu. Mhe. Jacob ameyasema hayo leo jijini wakati alipofanya ziara maeneo ya kawe ambapo kulikuwa na mgogoro juu kubadirishwa eneo la kuzikiwa na kwenda kuwa makazi ya watu.
Taasisi ya Mkapa imevamia kweli? Inaonekana imegawiwa.Inawezekana imegawiwa kwa makosa lakini napata taabu kuamini taasisi his imevamia.
ReplyDelete