Na Geofrey Chambua

Nyangumi ni mamalia wa bahari, au pengine wa maji matamu, wanaofanana na samaki ingawa hawatagi mayai kama samaki lakini huzaa watoto kama mamalia wote na huwanyonyesha. 

Pamoja na nguva wanyama hawa ni mamalia wa pekee wanaoishi kwenye maji tu. Oda yao ina mnamo spishi 80. Spishi ndogo huitwa pomboo kwa kawaida na spishi kadhaa za pomboo huishi kwenye maji matamu ya mito mikubwa kama Ganges au Amazonas.

Hizi ni Baadhi ya Tu ya Dondoo Kumhusu Nyangumi Baada ya Tafiti Mbalimbali


​1. Moyo wa nyangumi una kilo 600, ukubwa wake ni sawa sawa na ukubwa wa gari ndogo. Baadhi ya mishipa ya nyangumi ni mikubwa kiasi kwamba Binadamu anaweza kuogelea ndani ya mishipa hiyo bila kugusa pembeni

2. Mtoto wa nyangumi hun​yonya takribani​ lita ​6​00 ZA MAZIWA​  kila siku ​akiwa na umri wa miezi saba tu ​​huku akikadiriwa kuwa na uzito wa kilo 2700 ambayo ni sawa sawa na kifaru mkubwa size ya mwisho
3. Uzito wa nyangumi mkubwa unakadiriwa kuwa tani 200 hadi 300 ambapo ulimi wa nyangumi peke yake una uzito wa tani 3 ambao ni uzito zaidi ya Tembo mkubwa​.​

4. Mdomo wa nyangumi unaweza kuhifadhi tani 90 za chakula na maji akiufumbua mpaka mwisho

5. Urefu wa nyangumi unakadiriwa kuwa wa mita 30 mpaka 50, ukimuweka ardhini urefu wake ni sawa sawa na urefu utakaojitokeza baada ya kupanga ​kama basi moja hivi la mwendo kasi.​ ​

6. Nyangumi ndio mnyama mwenye sauti kubwa kuliko kitu chochote duniani ambayo inaweza kusikika mpaka umbali wa kilomita 848. (yaani akilia Dar anaweza kusikika hadi Mbeya)

7. Chakula kikuu cha nyangumi ni dagaa kamba, ambapo nyangumi mkubwa hula dagaa kamba zaidi ya 4000000 kwa siku, ili nyangumi ashibe vizuri anakula kilo 3600

8. Yasemekana Nyangumi anaweza kuishi mpaka kufikia miaka 80 hadi 90

9. Ukubwa wa nyangumi unaweza kulinganishwa na ndege aina ya Boeing 737

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Huyu unayemzungumzia hapa ni aina ya nyagumi aitwaye Ble whale kwa kiingereza. Na hawa ni wachache duniani na wako hatarini kupotea (endangered species).
    Quote:
    The blue whale is a marine mammal belonging to the baleen whales. At up to 30 metres in length and with a maximum recorded weight of 173 tonnes, it is the largest extant animal and is the heaviest known to have existed. Wikipedia
    Scientific name: Balaenoptera musculus
    Mass: 190,000 kg (Adult)
    Lifespan: 80 – 90 years
    Conservation status: Endangered (Population increasing) Encyclopedia of Life
    Gestation period: 11 months Encyclopedia of Life
    Trophic level: Carnivorous Encyclopedia of Life
    Length: Female: 25 m (Northern hemisphere population, Adult), Male: 24 m (Northern hemisphere population, Adult)

    ReplyDelete
  2. Kwa nini wanapotea hao? Wanavuliwa na wanadamu kwa ajili ya kitoweo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...