Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyesimama) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa juu ya mgogoro baina yao na pori la akiba la Mkungunero katikati ya Wiki (Juni 15, 2016).
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyesimama) akiwaonesha Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa Naakala ya tangazo la Serikali lililotangaza pori la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano wa kujadili mgogoro baina ya wanachi hao na pori la akiba katikati ya Wiki (Juni 15, 2016).
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Shaban Kissu (aliyesimama) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa juu ya mgogoro baina yao na pori la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa huo katikati ya Wiki (Juni 15, 2016).
Mzee Mathayo wa kijiji cha Ikengwa akiishukuru serikali ya Rais Magufuli kwa kuanza kushughulikia mgogoro baina ya wananchi wa kijiji hiko na pori la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma ambapo kamati iliyohusisha wananchi, Pori la akiba Mkungunero na Uongozi wa Wilaya Kondoa iliundwa kumaliza mgogoro huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...