Na Atley Kuni, RS Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amefanya ziara ya kushtukiza katika chuo cha Ufundi Buhongwa kwa lengo la kujionea utengenezaji wa madawati ambapo Halmashauri ya Jiji la Mwanza imepiga kambi katika eneo hilo kwa ajili ya madawati ya Wilaya ya Nyamagana.
Ziara hiyo imekuja ikiwa zimesalia siku ishirini na mbili kabla ya tarehe ya mwisho kwa mikoa kukabidhi takwimu za madawati kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, ambaye alitoa muda kwamba hadi kufikia tarehe 30, Juni, 2016 kila mkoa uwe umejitosheleza kwa madawati.
Akiwa katika eneo la tukio mkuu wa mkoa amewahimiza watengenezaji hao kuongeza bidii ili ifikapoa tarehe yakuwasilisha wawe wamekamili shughuli hiyo.“Nadhani  mnafahamu muda umekwenda, ni vema mkaongeza spidi yenu ya utengenezaji ili tuweze kumaliza kwa wakati kama mkoa kisha nasi tuweze kuwasilisha kama jinsi maelezo ya Mhe. Rais yalivyo  elekeza.
Kwa upande wake, mkufunzi katika chuo hicho ameahidi kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na kusema kama hali itakwenda vizuri basi kufikia tarehe 20, Juni watakuwa wamekamilisha “Tulikuwa na changamoto ya vyuma hapa katikati lakini hivi sasa tatizo hilo limekwisha na spidi yetu kama mnavyo iona niyakuridhisha”.
Mkoa wa Mwanza wenye mahitaji ya madawati 277,865 kwa takwimu za mwisho kabla yakuanza zoezi hilo ulikuwa unakabiliwa na upungufu wa madawati 168,354. Kukamilika kwa madawati hayo kutauwezesha mkoa kujitosheleza kwa kila shule mtoto kukaa juu ya daati.
 Gari, likiwa linapakia mawadawati ambayo yamekamilika kwa ajili yakupelekwa kwenye shule zenye upungufu.
 Mmoja ya watumishi kutoka Jiji la Mwanza, aliyekutwa eneo la Buhongwa, akisimamia shughuli ya utengenezaji wa madawati.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe John Mongella baada yakuwasili katika eneo la Buhongwa na hapo alikuwa akipokea maelezo juu ya shughuli zinavyo endelea katika Chuo hicho.
Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2016

    Kila mtu madawati.
    Mbona viatbu, madaftari, chaki, mabati, cement, kokoto hamtoi? Madarasa ya ziada yanahitajika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...