Na Geofrey Tengeneza
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally  Samatta (23) anayecheza kandanda la kulipwa katika klabu ya Genk nchini Ubelgiji amekubali ombi la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa Balozi wa hiari wa Tanzania na kusaidia kuitangaza Tanzania kama eneo la Utalii nchini Ubelgiji na Ulaya kwa ujumla.
Samatta ametoa ahadi hiyo leo alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii jijini Dar es salaam na kuwa na mazungumzo na Menejimenti ya Bodi hiyo kuhusu kumtumia katika kutangaza vivutio vya utalii na Tanzania kimataifa.
“ Kama mtanzania ninawiwa kwa nchi yangu hivyo nina furaha na niko tayari kitangaza nchi yangu kama eneo la utalii popote nitakapokuwa” alisema. Aliongeza kwamba nchi nyingi duniani hutumia watu wao maarufu ikiwa ni pamoja na wachezaji wa kimataifa kuzitangaza nchi zao.Ameipongeza Bodi TTB kwa mkakati wa kuwatumia watanzania mbalimbali maarufu katika kuitangaza Tanzania akaahidi kufanya kila litakalowezekana ikiwemo kutumia mitandao yake ya kijamii kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota mdachi amedokeza kuwa TTB itatazama namna nzuri kabisa ya kumtumia Mbwana Samatta kutangaza utalii wa Tanzania na Tanzania kwa ujumla kama eneo zuri kwa utalii.
Mbwana Samatta amesaini mkataba wa kuichezea klabu ya Genk ya Ubelgiji utakaomalizika mwaka 2020. Sammata ambaye ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa star, alitwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika.
Mbwana Samatta (katikati) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya TTB wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi hiyo Bi Devota Mdachi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...