Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KOCHA mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars", Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa anazifahamu mbinu zote wanazotumia timu za Ukanda wa kiarabu na ameshajizatiti kuweza kupata matokeo kwani ana wachezaji wa kila aina wanaoweza kutumia mfumo wa aina yoyote.
Stars wanakabiliwa na mchezo wa kufuzu kwenda kwenye fainali za mataifa Afrika AFCON 2017 wakiumana na Mafarao wa Misri mechi itakayopigwa kwenye dimba la uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mkwasa amesema kuwa, wachezaji wake wote wanajua umuhimu wa mchezo huo na wanataka kufungua ukurasa mpya katika historia ya soka la hapa nchini kwa kufuzu kwani kama wakifanikiwa kupata matokeo dhidi Misri na hilo linawezeka kama kipindi cha kwanza wakiweza kupata goli la kuongoza ambalo anaamini litawaondoa mchezoni.
"Tumejiandaa kikamilifu na kama tukipata matokeo kipindi cha kwanza tutawaondoa mchezoni na kikubw zaidi wachezaji wanajua kinachowapelekea na kama tukifanikiwa kushinda kwa goli tatu na zaidi tutapata nguvu zaidi ya kuwafunga Nigeria hata kama watakuwa nyumbani,"amesema Mkwasa. Najua Misri wamekuja na nia ya kutaka sare tu lakini wasione kama mechi hii itakuwa rahisi sana zaidi tunajua mbinu zao wanazotumia kipindi cha kwanza na hata cha pili.
Mkwasa ameweka wazi kwa watanzania wote kuja kwa wingi kwani kikosi chake kipo kamili kuwavaa mafarao hao na anataka kuvunja historia iliyokuwa inawasumbua kwa kipindi kirefu cha kufunga na mataifa ya kiarabu. Stars inawakilishwa na nyota kutoka Genk Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu kutoka TP mazembe ambao wameshajiunga na wenzao n tayari wameshakuwa fiti kuwakabili waarabu hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...