Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiongea mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati yapatayo 600 kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ili kuweza kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini. Makabidhiano hayo yalifanyika leo Juni 6, 2016 ofisini kwa mkuu wa mkoa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' kwa kuweza kutoa madawati 600 ikiwa ni mchango wake katika elimu ya kuweza kufanya wanafunzi kukaa sehemu salama. Mhe. Makonda alisema kuwa wakati umefika kwa wasanii wakaweza kujitoa katika jamii ambayo imekuwa ikiwapa wao sapoti na msanii Diamond amekuwa wa kwanza kuonyesha moyo wa pekee kwa kurudisha fadhila.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa WCB mara baada ya kumtembelea ofisini kwake.
Vichekesho Diamond katinga na vazi la Kinigeria
ReplyDeleteHili ni jambo zuri lakini kuna walakini,mbona hatuoni DAwati au walau hundi yoyote ile inayokabidhiwa kwa mkuu wa mkoa???zaidi ya kuona Abdul Nasib (Diamond )akiongea tuu.Nanyi waandish mwatakiwa kuwa makini kwani mnatoa taswira isiyo lingana na hali halisi.
ReplyDeleteNakubali ana na annony namba 1. Ametoa kiasi gani? Ili tufahamu thamini ya dawati moja. Aidha ndio uwazi na ufuatiliaji.
ReplyDeleteGood
ReplyDelete