Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimpongeza Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na kutoa mchango wake wa madawati yapatayo 600 kwa ajili ya kuchangia maendelea ya mkoa. Akiongea katika makabidhiano hayo msanii huyo alisema ni jambo jema kwao kuweza kujitolea mchango huo ili kuweza kumuunga mkono Mhe. Makonda katika kukabilana na changamoto za elimu.
Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiongea mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati yapatayo 600 kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ili kuweza kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini. Makabidhiano hayo yalifanyika leo Juni 6, 2016 ofisini kwa mkuu wa mkoa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' kwa kuweza kutoa madawati 600 ikiwa ni mchango wake katika elimu ya kuweza kufanya wanafunzi kukaa sehemu salama. Mhe. Makonda alisema kuwa wakati umefika kwa wasanii wakaweza kujitoa katika jamii ambayo imekuwa ikiwapa wao sapoti na msanii Diamond amekuwa wa kwanza kuonyesha moyo wa pekee kwa kurudisha fadhila.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa WCB mara baada ya kumtembelea ofisini kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2016

    Vichekesho Diamond katinga na vazi la Kinigeria

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2016

    Hili ni jambo zuri lakini kuna walakini,mbona hatuoni DAwati au walau hundi yoyote ile inayokabidhiwa kwa mkuu wa mkoa???zaidi ya kuona Abdul Nasib (Diamond )akiongea tuu.Nanyi waandish mwatakiwa kuwa makini kwani mnatoa taswira isiyo lingana na hali halisi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2016

    Nakubali ana na annony namba 1. Ametoa kiasi gani? Ili tufahamu thamini ya dawati moja. Aidha ndio uwazi na ufuatiliaji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...