Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akitangaza bungeni jDodoma jioni kwamba wabunge wa upinzani waliokuwa wakitoka bungeni posho zao zitakatwa kwa siku zote walizotoka.  Uamuzi huo uliotokana na muongozo uliotolewa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy, umeshangiliwa sana na wabunge wa chama tawala.

 Wabunge wa upinzani wakitoka bungeni muda mfupi kabla ya Bajeti ya Serikali kuanza kusomwa.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keisy (CCM), ambaye alitoa muongozo bungeni akitaka wabunge wa upinzani waliokuwa wakitoka nje kila mara wakatwe posho kwani wanalipwa bila kufanya kazi hivyo kuliingizia taifa hasara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2016

    Hivi hawa wabunge wa upinzani wanashindwa kujenga hoja za msingi ili kumwondoa Dk. Ackson kwenye kiti? Wananchi hawakuwatuma waende kuingia na kutoka mjengoni.
    Nchi inaongozwa na sheria. Kama wanaona Dk. Ackson hafuati sheria wajenge hoja na kutumia vyombo vilivyopo kumwondoa lakini hii ya kususa tu kila siku sio busara.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2016

    Kumuondoa haiwezekani hadi waungwe mkono na wabunge wa CCM kwa kuwa wapinzani ni wachache bungeni na maamuzi yanatolewa kwa wingi wa kura. Hapo inabidi watafute njia nyingine ya kupinga maamuzi sio kususa vikao wala kumuondoa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2016

    Hawana hoja yoyote ya msingi kwa sasa ndo maana wanataka kumtupia lawama naibu spika.Wao wanataka yale wayatakayo ndo yafuatwe hata kama yamekiuka kanuni na sheria za bunge.Ndo sababu kila mara wanataka kuomba muongozo kwa matukio yanayotokea na sio kujiandaa na jambo husika,mfano mzuri ni hili la Wanafunzi wa UDOM,kufukuzwa chuoni,walikurupuka na kuanza kuomba shughuli za bunge zote zisimamishwe ili kujadili,kitu ambacho hakipo kwenye ratiba na wala sio dharura ya kukatisha ratiba

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2016

    Shida hawa wanacheza na matukio. Wanapenda sana sifa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2016

    Hao ndio wabunge tuliowapeleka bungeni baada ya kutetea wananchi wanatoka nje sisi wapigakura hatufurahishwi na jambo hilo mshindane kwa hoja na si kwa kutoka nje kwani sharia ya bunge ikoje kama mbunge anasusia vikao zaidi ya mara tatu sisi wananchi hatuelewi Tunaomba hao wabunge watumie busara

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...