Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akitangaza bungeni jDodoma jioni kwamba wabunge wa upinzani waliokuwa wakitoka bungeni posho zao zitakatwa kwa siku zote walizotoka. Uamuzi huo uliotokana na muongozo uliotolewa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy, umeshangiliwa sana na wabunge wa chama tawala.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keisy (CCM), ambaye alitoa muongozo bungeni akitaka wabunge wa upinzani waliokuwa wakitoka nje kila mara wakatwe posho kwani wanalipwa bila kufanya kazi hivyo kuliingizia taifa hasara.
Hivi hawa wabunge wa upinzani wanashindwa kujenga hoja za msingi ili kumwondoa Dk. Ackson kwenye kiti? Wananchi hawakuwatuma waende kuingia na kutoka mjengoni.
ReplyDeleteNchi inaongozwa na sheria. Kama wanaona Dk. Ackson hafuati sheria wajenge hoja na kutumia vyombo vilivyopo kumwondoa lakini hii ya kususa tu kila siku sio busara.
Kumuondoa haiwezekani hadi waungwe mkono na wabunge wa CCM kwa kuwa wapinzani ni wachache bungeni na maamuzi yanatolewa kwa wingi wa kura. Hapo inabidi watafute njia nyingine ya kupinga maamuzi sio kususa vikao wala kumuondoa.
ReplyDeleteHawana hoja yoyote ya msingi kwa sasa ndo maana wanataka kumtupia lawama naibu spika.Wao wanataka yale wayatakayo ndo yafuatwe hata kama yamekiuka kanuni na sheria za bunge.Ndo sababu kila mara wanataka kuomba muongozo kwa matukio yanayotokea na sio kujiandaa na jambo husika,mfano mzuri ni hili la Wanafunzi wa UDOM,kufukuzwa chuoni,walikurupuka na kuanza kuomba shughuli za bunge zote zisimamishwe ili kujadili,kitu ambacho hakipo kwenye ratiba na wala sio dharura ya kukatisha ratiba
ReplyDeleteShida hawa wanacheza na matukio. Wanapenda sana sifa.
ReplyDeleteHao ndio wabunge tuliowapeleka bungeni baada ya kutetea wananchi wanatoka nje sisi wapigakura hatufurahishwi na jambo hilo mshindane kwa hoja na si kwa kutoka nje kwani sharia ya bunge ikoje kama mbunge anasusia vikao zaidi ya mara tatu sisi wananchi hatuelewi Tunaomba hao wabunge watumie busara
ReplyDelete