Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba, mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba na kuahidi kuyashughulikia. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omary Makame.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omary Makame, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba, mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mkutano huo umefanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.
Makamanda wa Jeshi la Polisi na waandishi wa habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni katika mkutano kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba, mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba. (Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...