Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo akimkabidhi kadi ya uanachama Goodluck Ole Medeye aliyekuwa mwanachama wa chama cha Demokrasia CHADEMA .
Na Woinde Shizza , Arusha
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi( UVCCM) umetabiri ipo idadi kubwa ya wanachama hasa vijana waliokumbwa na gharika ya kumfuata Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuhamia Chadema watakihama chama hicho kwasababu si taasisi kamili ya kisiasa ila ni kijiwe cha wasaka madaraka na vyeo .
Pia Umoja huo umesisitiza kuwa kuanza kuhama kwa Waziri zamani Goodlucky Ole Medeye ni mwanzo wa matayarisho ya vigogo wengine zaidi waliohamia chadema bila kukipima na kukipekua kiundani watajiondoa wakati wowote baada ya kuisoma namba.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Lengai ole Sabaya ameeleza hayo jana wakati akizungumza na wana wanachama wapya wa UVCCM na kuzindua shina jipya la wakereketwa katika kijiji cha Obalbal wilayani Ngorongoro Mkoani hapa.
Sabaya alisema kosa walilofanya baadhi ya viongozi na wanachama maslahi kuihama CCM kwa tashtit na mbwembwe anaamini kuwa siku zao sasa zinahesabika na wako njiani kujiondoa chadema huku baadhi yao wakitamani kurudi CCM ila milango ya kuingilia imefungwa kwa kuzuia usaliti na uasi .
Mwenyekiti huyo alifika katika kijiji cha Olbalbal kufuatilia iwapo wananchi katika kijiji hicho walipelekewa na serikali msaada wa mahindi ya chakula na kuwatosheleza.
Akizungumzia wanachama waliofuata mkumbo kwenda Chadema, alidai walifanya maamuzi ambayo si ya kizalendo , hayakutokana na tashwishi ya ukomavu wa imani yankisiasa wala kiitikadi ila walijikuta wakimfuata mtu kwa matumaini ya kupata na sasa wamejikuta wakipatikaana .
"Kuingia chama lazima mwanachama uwe na imani ya chama husika, sera zake, itiakadi na miongozo yake, waliokwenda Chadema hivi wamevutiwa na jambo lipi, mikuusanyiko, kuvaa magwanda au kusema mwaka huu hadi kitaeleweka" alihoji Sabaya.
Hata hivvo Mwenyekiti huyo aliwaeleza vijana katika kijiji hicho na kuwashitakia kwa wazazi wao kwamba wake na vijana wao wawaeleze kuwa maana ya kushika madaraka na kuongoza utawala ni lazima wapatikane viongizi wenye busara, hekima, maono, kipaji na uwezo wa kuiweka pamoja jamii bila mifarakano na migawanyiko.
Sabaya akisema iwapo vitu hivyo angepungukiwa navyo au mungu kutomjaalia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Dk Jakaya kikwete ,Taifa letu lisingepata sifa kimataifa ya kuwa ni tulivu , lenye umoja na ustawi wa amani.
Alisisitiza kuwa kwakuwa viongozi hao wote wamebahatika kuwa na upeo, maarifa na hekima ya kuzipima, kupembua na kutambua mabadiliko ya nyakati huku wakiwa na nia njema ndiyo maana waliiongoza Taifa kwa kufuata miiko, sera na maelekezo ya chama chao .
Alisema kuwa wale wote Waliopeperushwa na upepo wa kimbunga cha Lowassa kwanza wa subiri mpaka wao wajiridhishe kama bado ni wale wale au wamelishwa uasi na mioyo yao kama imeshiba uzalendo wa kutosha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...