Ule mchezo wa Saka saka unaoendeshwa na kituo cha Efm redio 93.7 namba ya bahati, leo siku ya Jumapili ya tarehe 19/06/2016 umewafikia wakazi wa Ilala pale kiwanja cha Aviation - Banana (Mamlaka ya anga),
Baada ya dondo la eneo husika na kitu husika kutajwa hewani wakazi wa Ilala hawakubaki nyuma bali kukesha wakisaka saka kidubwasha husika kilochofichwa, Huku washindi wakiibuka na shilingi milioni 3, ambapo mshindi wa kwanza ameibuka na kitita cha shilingi MILIONI 2.
Washiriki wakijaribu kubadilishana mawazo wakati wakisaka saka
Baadhi wa wakazi wa Ilala wakiwa wana saka saka kidubwasha kilichofichwa na Efm redio katika eneo la aviation pale Banana kitakacho mpatia mkwanja.
Haikujalisha mwanaume wala mwanamke wote walihusika katika zoezi zima la kusaka saka.
Moja kati wa washiriki akiondoka uwanjani akiwaacha washiriki wengine wakicheka baada ya kuwavunja mbavu wakati akipotoa kidubwasha chake kikaguliwe.
Washiriki wa wasaka saka wakiangalia na kushuhudia washindi waliofanikiwa kuibuka washindi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...