Serikali imeanza majadiliano na kampuni ya TING katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo uwanjani hapo.
Akizungumza
hapo jana wakati wa kikao kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo na kampuni hiyo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo
Bw. Alex Nkenyenge amesema kuwa Serikali imefarijika kupata maombi hayo
kutoka kampuni ya TING ya kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia
matangazo ambayo yatawekwa katika maeneo ya uwanja huo.
“Ndugu
zetu TING wamekuja na wazo zuri sana na tumelipokea na tunaahidi
kuliangalia kwa jicho la tatu kwani ni fursa ya pekee kwetu, sio
kuboresha mapato tu bali kutangaza uwanja wetu na kuendeleza michezo kwa
ujumla” alisema Bw. Nkenyenge.
Aliongeza
kuwa ni wakati sasa wa Serikali pamoja na Wananchi kufaidika na uwanja
wao ambao ni wa kipekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwani
fursa hiyo itasaidia pia kuendeleza Kijiji cha Michezo Changamani ambao
pia ni mpango wa Serikali katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos
amesema kuwa kampuni yake itatoa ushirikiano kwa Serikali kupitia Wizara
na ni azma yao kuona wananchi wanaona faida ya kuwa na uwanja wa kisasa
ambao utawaletea mafanikio katika maendeleo ya michezo nchini.
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Esther Yonael ameipongeza kampuni
ya TING kwa kuona fursa na kuitumia kwani kuna kampuni nyingi zinaweza
kuwa ziliona hiyo fursa hii lakini sikakosa uthubutu wa kuleta maombi
Wizarani kushirikiana katika suala hilo ambalo linafaida kwa pande zote
mbili.
Aidha,
Mkuu wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah ameihakikishia Serikali
kuwa wamejipanga vizuri na wamefanya utafiti wa kina wa mradi huo na
kuona kuwa unawezeka ukafanyika na kuleta mabadiliko katika sekta ya
michezo nchini.
Kampuni
ya TING imedhamiria kushirikiana na Serikali katika kuboresha mapato ya
uwanja wa Taifa na imejipanga kuwekeza Shilingi Billioni moja kwa miaka
minne katika miundombinu na wataalam.Serikali imeanza majadiliano na
kampuni ya TING katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia
matangazo uwanjani hapo.

minne katika miundombinu na wataalam.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza
na wawakilishi kutoka Kampuni ya TING(hawapo pichani) kuhusu
kushirikiana na Serikali kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia
matangazo.
Afisa
Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos akifafnua jambo
katika kikao kati ya kampuni yake na Serikali kilicholenga kushirikiana
katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
Mkuu
wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah akionesha jinsi kampuni yake
itakavyoweka miundombinu ya kuweka matangazo ndani ya uwanja wa taifa
katika kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika
kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
Baadhi
ya maafisa wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakifatilia
kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha
mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.(Picha na Raymond
Mushumbusi WHUSM)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...