Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati) na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba (kushoto) wakikata utepe ikiwa ishara ya makabidhiano ya magari matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini. Magari hayo yamekabidhiwa nje ya Jengo la Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia anayepiga makofi ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Thobias Andengenye.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akitoa hotuba fupi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuishukuru Serikali ya Japan kwa kuisadia wizara yake kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji magari tisa kwa ajili ya kazi ya kuzima moto na uokoaji nchini. Wa pili kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba akifuatiwa na Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Thobias Andengenye. Wa pili kulia ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Rogatus Kipali na Kamishna Msaidizi, Fikiri Salla. Tukio hilo lilifanyika nje ya Jengo la Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya magari tisa yaliyokabidhiwa na Balozi wa Japan, Masaharu Yoshiba kwa niaba ya Serikali yake yakiwa nje ya Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Magari hayo yaliyotolewa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yalipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara hiyo, Haji Janabi, jijini Dar es Salaam leo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...