SHIRIKA la Ndege la Etihad kupitia kitengo cha cha vifurushi, limeanzisha safari mbili kwa wiki ili kusafirisha mizigo kwa kutumia ndege ya A330 itakayotoa huduma zake kwenda Uwanja wa Ndege Brussels nchini Belgium kwa ajili ya kuimarisha shughuli za kiuchumi kati ya Abu Dhabi na Brussels na kongeza ufanisi wa huduma kwa wateja wake.
Ndege hiyo hutoa huduma ya usafiri mjini Brussels pia ikibeba mizigo, usafiri huo wa ndege ni muhimu kwa uchumi wa Belgium na Ulaya kwa ujumla.
Makamu wa Rais Kitengo cha Vifurushi wa Shirika la Ndege la Etihad, David Kerr alisema, “Brussels ni njia muhimu barani Ulaya kwa shughuli za usafiri wa ndege, ni eneo ambalo tumepanga kujitanua zaidi kwa mwaka huu, tunafurahia kuanzisha shughuli zetu ndani na nje ya mji huu. Brussels ni kiungo muhimu barani Ulaya na kiungo muhimu kwa Afrika, hivyo tunaamini itakuwa njia muhimu zaidi ambayo itaunganisha ulimwengu katika mtandao wa usafiri wa anga.”



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...