Familia ya Marehemu
Mzee Gaspar Theodore Mtonga wa Majumba Sita Dar es Salaam (pichani) inayoheshima kutoa
shukrani za dhati kabisa kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao walishiriki kwa
namna moja ama nyingine kufanikisha mazishi ya baba yetu mpendwa GASPAR THEODORE
MTONGA aliyefariki dunia Mei 2, 2016 katika hospitali ya Hindu Mandal na
Kuzikwa Matombo Morogoro Mei 6, 2016.
Kwa vile
waliotuunga mkono na kutufariji wakati wa kipindi hiki kigumu cha msiba ni wengi na ni vigumu kuwataja kwa
majina. Familia, inapenda kwa heshima na taadhima nyingi kutoa shukrani za
Jumla ikiwaomba kuzipokea shukrani hizo kwa moyo ule ule kama milivyo tuunga
mkono.
Hata hivyo
tunapenda kutoa shukrani za pekee kwa madaktari na wauguzi wote wa Hospitali ya
Arafa iliyopo Majumba Sita na Hindul Mandal ya Dar es Salaam. Tunashukuru
Uongozi wa SUMATRA Makao Makuu, Jeshi la Polisi Makao Makuu, Jeshi la Magereza
Makao Makuu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Parokia ya Kipawa na Wanajumuia ya Mtakatifu Maxmillian Kolbe Majumba Sita, Parokia
ya Mtakatifu Paul Matombo ikiongozwa na Baba Paroko Amselm Kobelo na Wanakwaya
wa Kanisa la Mtakatifu Paul Matombo. Majirani wote wa Majumba Sita na wa Kijiji
cha Mwangazi Matombo waliofika kutufariji.
Tunawashukuru
Sana.
Mungu Awabariki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...