Imeelezwa kuwa uelewa juu ya upatikanaji wa ardhi, Ushiriki wa wananchi
na ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaohamishwa ili kupisha mradi wa
bomba la mafuta litakalo jengwa kutoka kabaale nchini Uganda hadi Tanga
Tanzania vitachangia katika kufanikisha zoezi la upatikanaji wa ardhi na
kukamilisha shughuli za kimazingira kwa ajili ya ujenzi wa bomba hilo.
Hayo yameelezwa hivi karibuni mjini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna
wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Norbert Kahyoza wakati wa
Warsha iliyolenga kujadili upatikanaji wa ardhi na kutathimini athari za
Mazingira (EIA) ya ujenzi wa bomba hilo la mafuta kwa serikali ya
Tanzania na Uganda.
“Serikali kutoka pande zote mbili lazima tuwe makini kuhusu upatikanaji
wa ardhi, lazima wananchi wapate uelewa mzuri na waone uwepo wa
umuhimu wa bomba hili la mafuta na faidi zake kwani mradi huu ni
muhimu.” alisema mhandisi Kahyoza.
Aidha, Mkurugenzi wa Mkondo wa Chini kutoka Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. Wellington Hudson alieleza kuwa warsha
hiyo ya upatikanaji wa ardhi pamoja na masuala ya mazingira ni ishara
nzuri ya mwanzo katika utekelezaji wa mradi huo wa bomba la mafuta.
Vile vile mwakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini ya
Uganda, Francis Elungat alisema kuwa Waganda wamekuwa wakijiuliza ni
lini watafaidika na mafuta yao, hivyo amefurahishwa kuona kuwa mradi huo
uko mbioni kuanza hivyo wananchi wa Uganda kufaidika na mafuta yao.
Ujumbe kutoka Uganda wakifuatilia Mada zilizowasilishwa katika kikao cha wadau wa mafuta, kutoka kulia ni afisa Mwandamizi wa Mazingira, Jane Byaruhanga, wa pili ni afisa Mwandamizi wa Ardhi, Francis Elungat na afisa mwandamizi wa Ardhi Denis Karamagi.
Mchakato wa upatikanaji wa ardhi na kushugulikia masuala ya mazingira ni
hatua za awali za safari ya wananchi wa Uganda kupata faida za mali asilia
inchini mwao.
Aliongeza kuwa ujenzi wa bomba la mafuta na kiwanda cha kuchakata
mafuta hayo ni muhimu sana kwa wananchi wa Uganda na nchi nyingine
za Afrika Mashariki hivyo ni vema pande zote mbili zikubaliana katika hatua
zote za utekelezaji wa mradi huo.
Naye Meneja wa Mradi wa Kampuni ya Total Uganda, Jean Luc
Bruggeman, alisema kuwa ni lazima kuwepo na maelewano ya pamoja
kwa pande zote mbili juu ya nini kinahitajika na taratibu za upatikanaji wa
cheti cha mazingira (EIA) ili kuwezesha kuanza shughuli za ujenzi wa
mradi mapema, na kinachotarajiwa kufanyika kulingana na makubaliano ya
nchi hizo mbili na kuelewana nani atafanya nini katika mradi huo.
Wajumbe wakifuatilia mada katika kikao cha wadau wa Bomba la mafuta kilichofanyika katika hotel ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Warsha hiyo ilihudhuriwa na Ujumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Uganda, Kampuni ya Total E&P Uganda, wajumbe kutoka Halmashauri ya
Tanga, Bandari ya Tanga na Dar es Salaam, Shirika la Reli Tanzania,
Wizara ya Fedha, Wizara ya Ardhi, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi
wa Mazingira (NEMC),Chuo cha Ardhi, Tanroads, Ofisi ya Mwanasheria
Mkuuna Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...