Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel
Laurent (katikati), akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini
ya makubaliano ya ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari
zitakazojengwa na Watumishi Housing Company katika mikoa 23 ya Tanzania
Bara, ambapo familia 240 za walimu zitanufaika na ujenzi wa nyumba
hizo. Kushoto ni Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing
Company (WHC), Dk. Fred Msemwa na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango
na Uwekezaji wa TEA, Julius Rugemalila. (Picha na
Francis Dande)
Mkurugeni
Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa (katikati)
akizungumza wakati wa kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa
nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (kulia), akibadilishana hati na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari zitakazojengwa katika mikoa 23 ya Tanzania Bara, ambapo familia 240 za walimu zitanufaika na ujenzi wa nyumba hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (kulia) na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa wakipongezana.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...