TAREHE YA MWISHO KULIPA KODI YA MAPATO NA VAT

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawakumbusha walipakodi wote kulipa Kodi ya Mapato na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kabla ya tarehe 30 Juni 2016 ili kuepuka usumbufu na msongamano.

TRA pia inawakumbusha wafanyabiashara wote wa Dar es Salaam ambao mauzo ghafi ni kati ya shilingi millioni 14 na milioni 20 kwa mwaka kufika ofisi za TRA katika mikoa yao husika kuchukua mashine za EFDs kabla ya tarehe 30 Juni 2016. Baada ya tarehe 30 Juni, zoezi la kugawa bure mashine za EFDs katika mkoa wa Dar es Salaam litasitishwa. 

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja simu namba:

0800-780078 au 0800-750075 


Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
Mamlaka ya Mapato Tanzania
Dar es Salaam.


“PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2016

    Tulipe kodi tujenge taifa letu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...