Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam,Wakiingia katika eneo la Makao Makuu ya Vodacom Tanzania,Mlimani City kujipatia simu Orijino kwenye Gulio la siku mbili la simu lililoandaliwa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki, kampuni hiyo iliandaa gulio hilo kutokana na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima simu feki.
Mkazi wa jijini Dar es Salaam akiwa na mfuko ukiwa na simu Orijino baada ya kununua katika Gulio la siku mbili la simu,Lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Makao makuu ya kampuni hiyo,Mlimani City jijini Dar es Salaam jana, kampuni hiyo imeamua kufanya Gulio hilo kutokana na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) kuzima simu feki.
Baadhi ya Mawakala wa Vodacom Tanzania,wakimhudumia Aron Mwaifuge, baada ya simu yake kuzimwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA juni 16 mwaka huu, aliyefika kununua simu Orijino katika Gulio la siku mbili la simu lililoandaliwa na kampuni hiyo na kufanyika mwishoni mwa wiki katika Makao makuu ya kampuni hiyo,Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Wakala wa Kampuni Vodacom Tanzania, Rose Mery(kushoto) akiwasikiliza wateja waliofika katika banda lao wakati wa Gulio la siku mbili la kuuza simu Orijino lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Makao makuu ya kampuni hiyo,Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kampuni hiyo iliandaa gulio hilo kutokana na wateja wengi kuzimiwa simu zao feki na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...