Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Tanzania, Nasra Juma ametangaza majina ya wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Twiga Stars.
Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda Julai 15, 2016 kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda ikiwa ni mwaliko maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (Ferwafa).
Wakati Ferwafa likiingiza mchezo huo wa Julai 17, 2016 kwenye orodha ya michezo inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira na Miguu la Kimataifa (Fifa), lakini Mheshimiwa Rais wa Rwanda Paul Kagame kuwa sehemu ya burudani ya burudani mbele ya wageni wake ambao ni wakuu mbalimbali wanaounda Umoja wa Nchi za Afrika (AU) ambao watakuwa na mkutano wao nchini Rwanda.
Mbali ya soka kama burudani, pia Rais Kagame atatumia mchezo huo kama hamasa kwa wakuu wa nchi ili kutoa kipaumbele kwenye soka la wanawake ambako kwa sasa ni ajira ambayo inakwenda sambamba na kuitikia wito wa kupambana na changamoto za malengo ya millennia (MCC) ambayo pia yanataka wanawake wapate nafasi.
Makipa:Fatma Omary, ,Belina Julius, Najiat Abbas; Walinzi:Stumai Abdallah, Fatma Issa,Anastazia Antony, Happuness Henziron, Maimuna Khamis; Viungo:Donisia Daniel, Amina Ali, Amina Ramadhani, Fatuma Bashiri; Wema Richard, Fadhila Hamadi, Mwajuma Abdallah, Anna Hebron, Sophia Mwasikili; Washambuaji: Tumaini Michael, Johari Shaaban, Fatma Idd, Shelder Bonifdace Mafuru, Asha Saada Rashid na Mwanakhamisi Omar.
……………………………………………………………….

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...