Na Ally Daud-Maelezo
Wakala wa Majengo nchini (TBA) wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 2.6 sawa na asilimia 43 kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo wapangaji wa nyumba  hizo kushindwa kumalizia madeni wanayodaiwa
Akizungumza hayo katika kilele cha kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma nchini Mkurugenzi Mtendaji wa TBA Bw. Elius Mwakalinga amesema kuwa wamefanikiwa kukusanya kiasi hiko cha fedha kutoka kwa wateja wao waliowapangisha majengo na bado wanaendelea kukusanya mpaka watakapomaliza.
“Kutokana na mkakati wa kukusanya mapato na kutoa huduma bora kwa wateja wetu tumefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.6 katika kipindi cha miezi mitatu tuliyowapa wateja wetu  kuweza kukamilisha malipo hayo” alisema Bw. Mwakilinga
Mbali na hayo Bw. Mwakilinga amesema kuwa wameamua kutumia siku hiyo kufanya usafi kwenye makazi ya watumishi wa umma na wakazi wengine ili kuweka mazingira bora kwenye miradi yao na jamii nzima kwa ujumla.
“Siku ya leo tumeamua kuitumia kufanya usafi kwenye maeneo ambayo tumeweka miradi yetu kwa watumishi wa umma pamoja na mazingira mengine ili kuepuka na magonjwa yasababishwayo na uchafu” alisisitiza Bw. Mwakilinga.
Aidha Bw. Mwakilinga amesema wanampango wa kupanua wigo wa huduma yao kwa kuwapangisha watumishi  wa umma ambao wanastaafu waendelee kukaa kwenye nyumba hizo ili wasipate shida mara baada ya kustaafu. 
Mbali na hayo Mkurugenzi Mtendaji huyo amesisistiza kuwa  wataendelea na utaratibu wao wa kukusanya kodi  na kuchukua nyumba zao kwa  wale ambao wamekaidi amri yao ya kutolipia kodi nyumba hizo ili wapewe wengine ambao wana huitaji .
Wiki ya utumishi wa Umma imeadhimshwa  kwa kila taasisi ya kiserikali kusikiliza na kutatua kero zinazowapata wateja wanaoutumia huduma za taasisi husika ili kuipeleka nchi katika utendaji bora na mafanikio kwa ujumla.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Bw. Elius Mwakalinga wa kwanza kushoto akiwaongoza wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya usafi jijini Dar es salaam katika kuadhimisha kilele cha wiki ya utumishi wa Umma.
Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) wakishiriki katika kufanya usafi jijini Dar es salaam ili kuadhimisha kilele cha wiki ya utumishi wa Umma. Picha na Ally Daud-Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...