Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kulia) akipokea ndege maalum aina ya drones kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco Lambertini (wa tatu kushoto) kwa ajili ya kusaidia doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous. Wengine katika picha ni kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa WWF - Tanzania, Amani Ngusaru, Meneja wa Pori hilo la Akiba Selous, Mabula Misungwi, Mwenyekiti wa bodi ya WWF - Ujerumani, Dkt. Valentin Von Moscow, Mkurugenzi Mtendaji WWF – Ujerumani, Ebenhard Brandes na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuwia Ujangili, Faustine Ilobi Masalu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Viongozi wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) na Viongozi wengine wa Wizara wakipokea maelekezo kutoka kwa Mtaalam wa uendeshaji wa ndege maalum aina ya drones na jinsi zinavyofanya kazi, Parmena Elisa, ndege hizo zilitolewa na Mfuko wa WWF kusaidia doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous jana tarehe 1 Julai, 2016 Matambwe Selous.
Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya ndege maalum aina ya drones zilizotolewa na Mfuko wa WWF kusaidia doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco Lambertini (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji WWF – Ujerumani, Ebenhard Brandes (kushoto).
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...