Zaidi ya wakazi 55 kutoka mkoa wa Dar es salam na Pwani wamejishindia pesa taslimu zenye thamani ya shilingi milioni kumi na tano kupitia mchezo wa sakasaka ulioandaliwa na EFM redio.
Mchezo huu wa sakasaka ulianza tarehe 12/06/2016 katika wilaya ya kinondoni na kwenda katika wilaya ya Temeke, Ilala, Mkuranga na kumalizika leo tarehe 10/07/2016 katika wilaya ya Kisarawe. Wakazi zaidi ya kumi kutoka katika kila wilaya waliweza kusaka vitu vyenye thamani tofauti tofauti ya pesa kuanzia shilingi elfu hamsini hadi milioni mbili.
EFM redio huchezesha mchezo huu kila mwaka tangu redio ianzishwe kwa lengo madhubuti la kusaidia jamii inayotuzunguka, kwani pesa walizojishindia zitasaidia kuinua maisha yao kwa kufanyia biashara pamoja na kusaidia familia zao.
Mkazi wa Kimara-Temboni John Joseph akikabidhiwa pesa taslimu na meneja matukio na mawasiliano wa EFM redio Neema Godlays Mukurasi baada ya kusaka vitu vyenye thamani ya shilingi laki tatu. Wengine ni watangazaji wa kituo hicho cha redio kutoka kushoto ni Chogo akifuatiwa na Swebe Santana.
Mshindi mwingine akikabidhiwa pesa taslimu.
Mtangazaji wa EFM redio Chogo akimuhoji Bw. Sadam Raha mshindi wa shilingi milioni mbili wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani.
Umati wa watu walioshiriki kusaka saka vitu vilivyofichwa katika eneo hilo wakishuhudia washindi.
Baadhi ya washiriki wakisaka saka vitu vilivyofishwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...