Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka viongozi na watendaji wa chama hicho kuhakikisha mikataba ya kibiashara wanayofunga inapitiwa na kuwashirikisha wanasheria ili kuepuka vitendo vya utapeli.
Kimesema kuwashirikisha wanasheria wakati wa kufunga mikataba ya aina mbali mbali ya kukodisha Mali za Chama hicho kutasaidia kumaliza kero na migogoro ya matumizi mabaya ya Rasilimali za CCM.
Hayo aliyasema Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai katika mwendelezo wa ziara ya kukagua na kuhakiki mali za Chama hicho huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema matatizo ya matumizi mabaya ya Mali za chama hicho yanayojitokeza katika maeneo nchini ni kutokana na baadhi ya viongozi na watendaji kufunga mikataba ama makubaliano na wafanyabiashara bila ya kuwashirikisha wanasheria ama kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu hali inayopelekea baadhi ya watu kutumia nafasi hiyo kujinufaisha wenyewe badala ya kuangalia maslahi ya CCM.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...