Mpango
maalumu wa VSOMO unaotolewa kwa ushirikiano kati ya Airtel na VETA
unalenga kuwafikia vijana wengi zaidi katika kila kona ya nchi kupitia
simu za mkononi hivyo kuwapa urahisi wakazi wa mwanza na maeneo mengine
kupata nyenzo na mbinu muhimu katika biashara zao na kuwaandaa vyema
katika ushindani wa ajira ili kuinua uchumi wa viwanda wa Tanzania
Akiongea na wakazi wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella aliwapongeza VETA na Airtel kwa kuanziasha mpango huu wa VSOMO kwa wakati muafaka. Alisema “mpango huu ni wakibunifu na umekuja wakati muafaka kwani utawawezesha vijana kupata masomo ya kiufundi ambayo yachochea kukua kwa uchumi wao. Hivyo nawaomba VETA na Airtel wahakikishe VSOMO inaendelea kuwa mpango bora utakaosaidia watanzania kupata vijana wengi wenye taaluma kwaajili ya kuendesha uchumi wa viwanda na kunufaika na ajira zitakazotokana na kufanya vizuri kwa viwanda hivyo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza alitoa wito kwa vijana wa mkoa huo kutumia fursa hii kwa kujiunga na masomo ya VETA kupitia VSOMO. Alitoa shukrani zake na kusema “ Tunafurahi kwa Mwanza kuwa kati ya mikoa iliyopata nafasi ya kushuhudia uzinduzi huu kati ya VETA na Airtel. Nawapongeza kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha tunawawezesha watanzania kupata elimu bora na ujuzi zaidi kupitia VSOMO.
Kwa upande wake, Meneja huduma kwa jamii wa Airtel , Bi Hawa Bayumi alisema “ katika kutekelea za huduma zetu za jamii kwa nchini Airtel imedhamiria kuwawezesha na kuwaendeleza vijana kujikwamua kiuchumi kupitia program zetu. Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kutengeneza suluhisho la kibunifu kupitia simu za mkononi ambalo limeleta tija kwa jamiii kama vile VSOMO kwaupande wa msomo ya ufundi kwani VSOMO inawawezesha wateja wa Airtel kupata ujuzi na maarifa kupitia viganja vyao”
Akiongea kuhusu VSOMO, Mkuu wa chuo cha VETA kipawa Eng. Lucius Luteganya, alisema “ kuanzishwa kwa mfumo huu wa VSOMO kutachochea mabadiliko makubwa yatakayotoa nafasi kwa watanzania kutumia mpango huu wa kipekee kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na kwa gharama nafuu mahali popote kwa kutumia simu zao.

Huu
ni mpango wa kipekee Afrika mashariki na kati kwa kuwa hakuna taarifa
zinazoonyesha mfumo kama kuna application yenye kutoa mafunzo ya ufundi
duniani. wazi kabisa kukuwa kwa uchumi wa viwanda kutazidi kukua
kutokana na upatikanaji wa elimu za ufundi kwa uhakika na urahisi na
hivyo kushukuru kwa ushirikiano ulianzishwa kati ya VETA na Airtel
unakaosaidia utekelezaji wa mpango wa viwanda wa serikali ya awamu ya 5
Kozi vinazotolea kupitia application ya VSOMO kwa sasa ni pamoja Misingi Ya Ufundi Wa Pikipiki, Kuweka Umeme, Ufundi Wa Simu, Kuchomelea Na Kuunda Vyuma na Urembo Kozi hizi zinatolewa kwa gharama ya shilingi 120,000, muda wa kufanya mafunzo ya vitendo baada ya kufaulu masomo kwa njia ya mtandao ni masaa 60. Hii inamaanisha kwa aliyedhamiria kushoma itamchukua mwenzi moja kumaliza masomo yake kupitia VSOMO.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa Mwanza katika kijiwe cha waendesha bondabonda wakati alipokwenda kuzindua mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mkononi yajulikanayo kama VSOMO yanayoletwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwa wakazi wa Mwanza. Pichani ni wafanyakazi wa Airtel na VETA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella akimpatia vipeperushi mmoja wa kijana katika kijiwe cha Bodaboda mkoani Mwanza wakati alipokwenda kuzindua mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mkononi yajulikanayo kama VSOMO yanayoletwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwa wakazi wa Mwanza

Meneja huduma kwa jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella mara baada ya kumtembelea ofisini kwakwe na kutambulisha fursa zinazopatikana kwa wakazi wa mwanza kupitia mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mkononi ujulikanayo kama VSOMO unayoletwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...