Na Editha Karlo,wa blog ya jamii ,Muleba.


 SHEIKH wa Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera Sheikh Zakaria Mussa amewaomba waumini wa dini ya kiislamu kusamehe katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani.

Sheikh aliyasema hayo jana kwenye viwanja vya bank ya CRDB tawi la Muleba wakati wa futari iliyoandaliwa na bank hiyo kwa wateja na wafanyakazi wake.

Alisema kuwa japo mwezi mtukufu unaelekea ukingoni kuisha,lakini waumini wa kiislamu wanapaswa kujua huu ni mwezi wa toba hivyo watu wote wakae karibu na mwenyezi Mungu wakumbuke kusameheana pia wasimame katika imani.Sheikh Zakaria aliupongeza uongozi wa bank ya CRDB tawi la Muleba kwakutambua umuhimu wateja wao na kuwaandalia futari ya pamoja.

"Hawa ndugu zetu CRDB mbali na kutupatia huduma bora za kibenki lakini leo pia wametuonyesha wanatujali wateja wao na wamefanya jambo zuri la kutupatia futari leo"alisema."Mimi nawatakia kila la kheri katika kutimiza majukumu yao ya kila siku ya kutupatia huduma bora zenye viwango vya hali ya juu"alisema Sheikh

Meneja wa bank ya CRDC tawi la Muleba Hezron Ikilesho aliwashukuru wateja wa bank ya CRDB tawi la Muleba kwa ushirikiano wao na kuamua kuchagua bank hiyo kuweka fedha zao mahali salama."Bank yetu inawathamini sana wateja wake na ndiyo maana jioni ya leo tumejumuika pamoja katika futari hii na wateja wetu ,karibu tuendelee kuwahudumia"alisema

Naye Saada Juma mteja wa bank ya CRDB aliupongeza uongozi wa bank kwa kutambua umuhimu wa mahitaji ya jamii na kuanzisha akaunti mbali mbali kwa wateja wao."Naipenda bank ya CRDB kwakuwa fedha zangu zinakuwa salama ninapoweka,pia bank hii inajali jamii zote wameanzisha akaunti ya watoto,akaunti ya wanawake(malkia akaunti)"alisema mteja huyo.


Wateja wa bank ya CRDB Tawi la Mubela wakipata futari iliyoandaliwa na bank hiyo. 

Sheikh wa Wilaya ya Muleba Zakaria Mussa akitoa neno la shukrani kwa bank ya CRDB rawi la Muleba baada ya futuru
 

Meneja wa bank ya CRDB tawi la mleba(mwenye kanzu nyeupe)akifuturu na wateja wake wa CRDB tawi la Muleba.

Wateja wa bank ya CRDB Tawi la Muleba wakipata futari iliyoandaliwa na bank hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...