Mdau mwandamizi wa Globu ya Jamii Mhe. Mariam Mungula ni mmoja wa wasomi  ambao Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amewakubali na kuwaapisha kuwa Mawakili wapya. Jumla yao ni  624 na wameifanya Tanzania kuwa na jumla ya Mawakili 5800 kwenye sherehe iliyofanyika Ijumaa katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Wakili Mariam, ambaye ni mmoja wa wana-Diaspora walioamua kurejea nyumbani kuendeleza libeneke baada ya kuishi Ughaibuni (yeye alikuwa Uingereza) kwa miongo kadhaa, ameiambia Globu ya Jamii kwamba hajutii uamuzi wa kurejea nyumbani ambako amesema amekuta kuna fursa kibao za kimaendeleo kuliko wengi wanavyofikiria. Tunakupongeza sana daad Mariam kwa juhudi zako na moyo wa kizalendo.
 Mdau mwandamizi wa Globu ya Jamii Mhe. Mariam Mungula akisubiri kula nondozzz yake na wenzie. Idadi ya Mawakili inaendelea kuongezeka ambapo mwezi Desemba mwaka huu Mahakama inatarajia kuwaapisha mawakili wengine zaidi ya 300. Kwa  upande wa Afrika Mashariki, Kenya inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mawakili ambapo ina zaidi ya Mawakili 14,000.  Uganda kwa upande wake inayo mawakili 2500.

 Mdau mwandamizi wa Globu ya Jamii Mhe. Mariam Mungula na wenzie wakijipanga tayari kwa picha ya pamoja
Mdau mwandamizi wa Globu ya Jamii Mhe. Mariam Mungula akiwa na mdogo wake Hajra Mungula ambaye pia ni wakili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...