Illikuwa ni mtanange wa kufa mtu kwenye michuano ya Kombe la Ulaya (EURO 2016) inayoendelea nchini Ufaransa, kati ya Ubelgiji na Wales katika dimba la Stade Pierre-Mauroy. Mchezo ulianza kwa kasi na nguvu kwani dakika ya 5 tu Mwamuzi wa mechi hiyo Damir Skomina wa Slovenia alimzawadia kadi ya njano mchezaji Ben Davies wa Wales kwa kumfanyia obstraction Kelvin De Bruyne wa Ubelgiji.

Walikuwa ni Ubelgiji walioanza kujipatia bao la uongozi dakika ya 12 pale Radja Nainggolan alipoachia shuti kali nje ya 18 na kwenda moja kwa moja kimiani.Wales walikuja juu na kufanya mashambulizi ya hapa na pale,Ubelgiji wakijibu na kunako dakika ya 31 kona murua iliopigwa na Hal Robson-Kanu ikaunganishwa vizuri kwa kichwa na Ashley Williams akiipa Wales bao la kusawazisha. Hivyo hadi mapumziko timu zote zilikuwa zimefungana bao 1-1.

Ngwe ya pili ilianza kwa kasi na kuwachukuwa Wales dakika 10 kuhanikiza bao la pili lililowekwa kambani na mchezaji Hal Robson-Kanu aliyepokea pasi safi toka kwa Aaron Ramsey akawatambuka mabeki watatu wa Ubelgiji na kupiga mchomo mkali kwa mguu wa kushoto...moja kwa moja wavuni.
Ingawa Ubelgiji walijitahidi sana kutaka kusawazisha kwa kuliandama lango la Wales lakini waliambulia patupu kwani dakika ya 86 Sam Vokes wa Wales alishindilia msumari wa mwisho kwa kuipatia timu yake goli la 3, alifunga goli hilo kwa kichwa cha kiufundi zaidi huku akimuacha kipa wa Ubelgiji Thibourt Courtois akichumpa bila mafanikio. Kipyenga cha mwisho kilipopulizwa Wales 3 - Ubelgiji 1. Sasa Wales watakutana na Ureno katika nusu fainali ya kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...