Huduma ya 2 ya treni ya Jiji kutoka Pugu kwenda kituo kikuu cha Dar es Salaam kuanza kesho Jumatatu Agosti 01, 2016 saa 12 asubuhi.

Aidha taarifa Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL ) inafafanua huduma hiyo ya majaribio ya siku 2 Jumatatu na Jumanne itakuwa bure kwa Wakazi wa vituo husika.

Vituo hivyo pamoja na Pugu stesheni ni Mwisho wa Lami, Gongo la mboto, FFU Mombasa, Banana (Njia panda Segerea) na Karakata. Vingine ni pamoja na Vingunguti Mbuzi, SS Bakhressa, Kamata na Kituo kikuu cha reli Dar es Salaam!

Huduma hiyo itakuwa ya awamu 2 ya safari 3 kila awamu. Safari ya kwanza ya awamu ya 2 itaanza saa 9:55 Alasiri kutoka Dar stesheni.

Wito unatolewa kwa Wasafiri wa treni hiyo kuzingatia maelekezo ya Maafisa wa TRL watakaosimamia safari hiyo ya majaribio na kutoa ushirikiano kikamilifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...