Na Allan Ntana, Sikonge

BARAZA la Madiwani la halmashauri ya wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora limewafukuza kazi watumishi watatu wa halmashauri hiyo huku mmoja akisubiri kufikishwa mahakamani na wengine nane wakipewa onyo kali.

Akitangaza uamuzi huo, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Peter Nzalalila alitaja watumishi waliofukuzwa kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uzembe kuwa ni aliyekuwa Afisa Ushirika wa halmashauri hiyo Justin Kapufi, Afisa Sheria wa halmashauri Rebecca Liyanga na Mtendaji kata ya Kipanga Emmanuel Kalumay.
Aidha alisema Mweka Hazina wa halmashuri hiyo Evance Shimdoe na Mhasibu Richard Ndalo waliokuwa wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi baraza hilo limejiridhisha pasipo shaka kuwa watumishi hao walifanya uzembe katika utendaji wao hivyo kupewa onyo kali.

Katika maamuzi hayo aliyekuwa Afisa Utumishi wa halmashauri hiyo Elly Aketch ambaye alikumbwa na rungu hilo na kusimamishwa kazi awali, Mwenyekiti alisema halmashauri inaandaa utaratibu wa mashataka ili kufikishwa kizimbani kwa uzembe ulioisababishia hasara kubwa halmashauri hiyo.

Aliongeza kuwa aliyekuwa Mganga Mkuu Mfawidhi wa zahanati ya Kitunda Dk.Fredrick Mtao, Mtendaji wa kata ya Kitunda Ally Kicko, Mtendaji kata ya Kipanga Emmanuel Kalumay, Afisa Mipango miji wa Halmashauri Emmanuel Magembe wao wamepewa onyo na kutakiwa kuwa makini katika utendaji wao.

Aidha Watendaji Kata 4waliokuwa wamesimamishwa kwa tuhuma za upotevu wa vitabu vya kukusanyia mapato ya halmashauri wamepewa onyo kali na kutotakiwa kurudia uzembe wa aina hiyo kwani walichangia kwa kiasi kikubwa kupata hati yenye mashaka huku Godfrey Sungura shauri lake likiendelea kuchunguzwa kutokana na uzito wake.

Baada ya kusoma maamuzi hayo, Nzalalila aliwataka watumishi wote wa halmashauri na ujumla kwa ujumla kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na maadili ya kazi zao ili kuepuka kutumbuliwa jipu.

Aidha aliwataka kwenda na kasi ya Rais wa serikali ya awamu ya tano kwa kuwajibika ipasavyo huku wakitumia utaalamu wao kwa manufaa ya wananchi na aliahidi kuendeleza tumbuatumbua kwa watumishi wote wasiotaka kubadilika kiutendaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...