Kampuni ya Tracto Co Ltd ni Wasambazaji rasmi wa Cummins Filtration ( Fleetguard ) na
vilainishi vya Magari na Mitambo aina ya Valvoline nchini Tanzania.
Dhamira ni
usambazaji wa bidhaa bora ili kuruhusu wasimamizi na wamiliki wa magari na
mitambo kupunguza gharama za uendeshaji huku wakizingatia ubora. Timu ya
wataalamu kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Cummins na Valvoline hufanya kazi
bega kwa bega na watumiaji wa mwisho wa bidhaa hizo kuhakikisha wanaitumia bidhaa
kwa ufasaha na kuepuka majanga yatokanayo na utumiaji wa bidhaa hafifu.
Utendaji umejengwa juu ya nguzo 4 ambazo ni:
Uchujaji/Filtration - Kuondoa Uchafu kutumia Bidhaa bora duniani kama - Fleetguard ,
MANN na PALL.
Vilainishi/Lubricants – Kampuni ya Tracto Co Ltd wanasambaza vilainishi bora kutoka Valvoline na Lubrication
Engineers. Hivi ni vilainishi visivyokuwa na uchakachuaji wowote, wanakupa ubora
uleule ulio pendekezwa na wazalishaji wa vyombo vyote vya moto.
Uhifadhi wa Mafuta – Hii hufanyika kwa kutumia matanki imara kabisa yaliyojengwa
kwa kuta mbili, na huwekwa juu ya aridhi hivyo kurahisisha usafishaji na pia kurahisisha
usafirishaji iwapo unataka kuhama, vivyo hivyo kuweza kugundua itilafu yoyote ikitokea
katika tanki.
Uchunguzi na ufuatiliaji – Tunafanya Uchunguzi na Ukaguzi wa Mafuta kuona
kiwango cha Usafi wake, na Kutoa ushauri kuhusu nini unatakiwa kukifanya kama
mafuta yako tayari yana uchafu.
Afisa Mkuu wa Masoko ndg. Victor Ndamugoba akielezea bidhaa zao kwa watu waliofika kwenye banda lao (hawapo pichani).
Watu waliopata nafasi kutembelea banda la Tracto wakipata maelezo kutoka kwa wataalam kutoka Tracto.
Martin
(mwenye nguo nyekundu) mtaalam wa vilainishi kutoka Valvoline akisiliza
swali kwa makini kutoka kwa mmoja wa mteja aliyepita kutembelea banda
la Tracto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...