Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kumalizika kwa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume ni mwanzo wa safari ndefu ya mafanikio kwa Zanzibar katika azma yake ya kuitumia Sekta ya Utalii kuwa muhimili wa Uchumi Mkuu wa Visiwa vya Zanzibar.
Alisema azma hiyo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelenga kutafuta njia nyengine mbadala za kukuza uchumi wake na mapato ya Taifa ambayo kwa sasa yanaendelea kutegemea zao moja tu la karafuu.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Uongozi wa juu wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi { BCEG } ambayo ndio inayojenga eneo la maegesho ya Ndege kwenye Uwanja wa ndege wa Zanzibar kwenye Makao Makuu yake Jengo la Jian Geing laza Mjini Beijing Nchini China.
Akimalizia ziara yake ya siku Tano Nchini Jamuhuri ya Watu wa China akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif alisema ongezeko la idadi ya Watalii wanaoingia Zanzibar kwa sasa ni vyema ikaenda sambamba na uimarishwaji wa sekta hiyo muhimu kwa wakati huu.
Balozi Seif aliueleza Uongozi huo wa juu wa BCEG ukiongozwa na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Bwana Fan Jun kwamba Kampuni na Taasisi za ujenzi za China kutokana na umakini wake katika kazi zitaendelea kushirikishwa na Serikali katika uimarishaji wa miundombinu tofauti ya Maendeleo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza watendaji na Uongozi mzima wa Kampuni ya Ujenzi ya BCEG kwa kazi kubwa wanayotekeleza katika ujenzi wa miradi mikubwa ya mawasiliano akiitolea mfano ile ya Bandari na Viwanja vya Ndege.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushoto akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya BCEG Mhandisi Fan Jun Kushoto kwenye Makao Makuu ya Kampuni hiyo Jengo la Jian Going laza Mjini Beijing Nchini China.
Meneja Mkuu wa Shirika la Bima la China (SINO SURE) Bwana Wu Han Kulia akibadilishana mawazo na Balozi Seif mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Mjini Beijing.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa Pili kutoka Kushoto akiwa na Ujumbe wake akizungumza na Uongozi wa Shirika la Bima la China (SINO SURE) Mjini Beijing akimalizia ziara ya siku Tano Nchini China.
Balozi Seif Kati kati walioko mbele akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Juu wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya BCEG mara baada ya kumaliza mazungumzo yao ya ushirikiano. Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Meneja wa Kampuni ya BCEG Bwana Yongchun Chang, Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar DSr.id Salum Mohamed, Katibu Mkuu wake Nd. Khamis Mussa, wakati upande wa kulia ya Balozi Seif ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya BCEG Mhandisi Fan Jun na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum na Msaidizi Meneja wa BCEG wa masuala ya Kimataifa Bwana Shulong Ma. Picha na –OMPR – ZNZ.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...