Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix J. Lyaniva ametoa
wito kwa Watanzania kujivunia bidhaa za Tanzania kupitia viwanda vyetu nchini, akisistiza kuwa Tanzania ina viwanda vinavyoweza kuzalisha bidhaa za kwetu na wananchi wajifunze
kujivunia na kutumia bidhaa zetu wenyewe ili kukuza uchumi wa
viwanda.
Hayo ameyasema akiwa mgeni rasmi
kwenye makabidhiano ya nyenzo za ushonaji kwa wasiiona wanaoendelea na mafunzo
maalum ya ushonaji yanayoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
Mhe Lyaniva aliongeza kwa
kusema tarehe 7 hadi 11 Desemba katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere kutakuwa na
Maonesho ya Viwanda vya Tanzania, na katoa wito kwa wananchi waje waone viwanda vya Tanzania na
bidhaa zinazolishwa Tanzania wakiwemo wasioona wanaopata mafunzo maalum ili
watambue uwezo wao wa ukuzaji wa uchumi wa viwanda.
Bw Shadrack Nkelebe, Meneja wa
kiwanda cha nguo cha Urafiki amesema wamedhimiria kufanya kazi kwa karibu na Bw
Abdallah Nyangalio anapoendelea kutoa mafunzo. Amesema kwa nafasi yao ya uzalishaji
wanavyo vitenge na khanga za kutosha hivyo wanatoa ili kusaidia mafunzo maalumu ya ushonaji
kwa wasioona maana kazi wanayofanya ni nzuri na yenye manufaa kwa taifa maana
yanaleta maendeleo.
"Wakati
wa maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) tulivutiwa
sana na utendaji kazi wake lakini ni fundisho kwetu kwamba haya yanawezekana", alisema.
Nae Bw Abdallah Nyangalio
mkufunzi na mlemavu wa macho wakati akipokea nyenzo hizo ameshukuru kupatiwa vifaa hivyo ambavyo vitamwezesha
katika mafunzo yao na ana imani watafika mbali na kwamba tangu waanze mafunzo hayo tarehe 19 mwezi Oktoba, 2016
wanafunzi wamepiga hatua kubwa
Kaimu Mkurgenzi wa TanTrade Bw Edwin Rutageruka, amemshukuru Mkuu wa Wilaya
ya Temeke na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha URAFIKI kwa msaada wa nyenzo (Cherehani kutoka kwa Mkuu wa
Wilaya na Majora kutoka Urafiki ) ambazo zitawasaidia katika mafunzo maalum ya
ushonaji kwa wasiiona.
"Lengo la Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ni
kuhakikisha baada ya mafunzo hayo walemavu hawa wasioona watafutiwe na kupata masoko
ya ndani na je ya nchi", alisema na kutoa wito kwa wananchi waje kuona kiwanda cha
mlemavu asiyeona katika kipindi hicho cha maonesho ya
viwanda vya Tanzania maana atashiriki.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix J. Lyaniva akikakata utepe kama ishara ya kukabidhi msaada wa cherehani kwa Bw. Abdallah Nayngalio ambaye ni mkufunzi asiyeoona anayetoa mafunzo maalum kwa ya ushonaji kwa wasioona yanayoratibiwa na Mamlaka ya Maendelo ya Biashara Tanzania (TanTrade). Kulia ni Bw
Edwin Rutageruka, Kaimu Mkurgenzi wa TanTrade akifuatiwa na Meneja Mkuu wa kiwanda cha URAFIKI Bw Shadrack Nkelebe.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix J. Lyaniva akishuhudia Meneja Mkuu wa kiwanda cha nguo cha URAFIKI Bw Shadrack Nkelebe akimkabidhi majola ya vitenge kwa Bw Abdallah Nyangalio ambaye ni mkufunzi asiyeoona anayetoa mafunzo maalum ya ushonaji kwa wasioona yanayoratibwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade). Kulia ni Bw Edwin Rutageruka, Kaimu Mkurgenzi wa TanTrade. Habari na picha na Theresa Chilambo wa TanTrade.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...