Mashindano ya kuogelea ya klabu ya Dar es Salaam Swimming Club (DSC) yamepangwa kuanza Desemba 9 mpaka 10 kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Heaven of Peace Academy (Hopac).
Mashindano hayo ambayo ni ya kwanza kwa klabu ya DSC kuandaa, yatashirikisha waogeleaji zaidi ya 200 kutoka klabu mbalimbali za hapa nchini na nchi za Afrika Mashariki.
Katibu Mkuu wa DSC Inviolata Itatiro alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea na yatashrikisha waogeleaji wenye umri kati ya miaka chini ya sita, saba, nane, tisa, 10 mpaka 13.
Inviolata alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kutambua na kukuza vipaji kwa waogeleaji chipukizi ambao kwa manufaa ya nchi na hasa timu ya Taifa.

Alisema kuwa mchezo huo kwa sasa unakuwa kwa kasi na wao kusukumwa na mwamko huo kwa kuandaa mashindano hayo kwa vijana chipukizi.
“Mashindano haya ni moja ya kuendeleza mchezo huo, kuna waogeleaji wengi chipukizi ambao wanahiataji mashindano ya mara kwa mara ili kupina uwezo na kukuza vipaji vyao, tumeona umuhimu wa kuandaa mashindano haya kwa lengo hilo,” alisema Inviolata.
Alisema kuwa klabu yao imekuwa mstari wa mbele kuendeleza mchezo huo kwa kufundisha watoto, vijana wa umri wa kati na watu wazima kwa lengo la kuwafanya wapende mchezo huo.
“Nawaomba viongozi wa vilabu na makocha kuwa makini na umri wa waogeleaji wao, tunataka kuona waogeleaji wanashindana katika umri halisi, siyo kushindanisha wenye umri tofauti, hatutafikia lengo ambalo tumeliweka,” alisema Inviolata.
Alisema kuwa kutakuwa na washidi wa jumla ambao watapewa vikombe na mshindi mmoja mmoja katika kila kipengele ambao watapata medali kuanzia ya dhahabu, fedha na shaba. Pia kutakuwa na vyeti vya kutambua vipaji kwa waogeleaji.
Waogeleaji wa Dar Swim Club wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushinda mashindano ya Morogoro hivi karibuni.

Waogeleaji wa Dar Swim Club wakishindana katika moja ya mashindano hivi karibuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...