Na Dotto Mwaibale
Bohari kuu ya dawa (MSD) imezindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wake wakubwa, kama moja ya hatua za kuboresha huduma zake 
Mpango huo utawawezesha wateja hao kupata huduma ya haraka zaidi pindi wanapokuwa wanahitaji mahitaji yao.
Wateja hao ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Hosipitali ya Sekoutoure Mwanza, Hospitali ya Kibong’oto, Mirembe, Hosipitali za Amana, Temeke, Mwananyamala, KCMC, Hospitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Akizindua mpango huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya amesema mpango huo ni moja ya maboresho yanayofanywa na MSD, ili kuhakikisha huduma zake zinatolewa kama inavyohitajika.
Dk. Mpoki pia amewasisitiza wateja hao wakubwa wa MSD kuhakikisha wanafanya maoteo sahihi ya mahitaji yao na kuyaleta MSD kwa wakati ili kuepusha ucheleweshwaji wa taratibu za manunuzi ambao pia itasababisha dosari kwenye upatikanaji wa dawa kwa wateja. 
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu  amesema hatua ya kuwahudumia wateja hao kwa kiwango kizuri na cha uhakika itafanikiwa, hivyo Watarajie maboresho makubwa ya huduma ya upatikanaji wa dawa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  Profesa Mohamed Janabi (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunu (kulia) akitoa taarifa fupi ya mradi huo 
Meneja Huduma kwa Wateja wa MSD Bi. Salome Malamia akizungumza katika hafla hiyo.
Mmoja wa maofisa kutoka Ofisi inayosimamia Utekelezaji wa Mapendekezo ya Maboresho (SMO),  Bi. Naomi Shangali akitoa maelezo kuhusu mpango huo.  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...