Na Jacquiline Mrisho
– MAELEZO.
– MAELEZO.
Mbali na jitihada za makusudi za Serikali na
wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI nchini bado hali siyo ya kuridhisha ambapo
Jiji la Dar es Salaam linashika nafasi ya Sita barani Afrika kwa maambukizi ya
ugonjwa huo.
Dar es Salaam ambalo ni Jiji kubwa kuliko
yote Tanzania linakadiriwa kuwa na watu 210,000 wanaoishi na virusi vya UKIMWI
ambapo kati yao asilimia 58 ni wanawake, na kwa mujibu wa sensa ya watu na
makazi ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wa jiji hilo inakadiriwa kuwa Milioni 5.
Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya UKIMWI duniani
kutoka Shirika la Mpango wa UKIMWI la Umoja wa Mataifa - Tanzania (UNAIDS) kwa
mwaka 2015, Jiji la Dar es Salaam limekuwa kati ya majiji Barani Afrika yenye
kiwango kikubwa cha maambukizi ya UKIMWI.
Afisa wa UNAIDS Tanzania, Fredrick Macha (pichani) anasema asilimia 16 ya maambukizi yote mapya Tanzania
Bara yanatokea katika jiji la Dar es Salaam ambapo kwa wanawake wenye umri
mdogo wa miaka 15-24 kiwango cha maambukizi kimefikia asilimia 7%,sababu kubwa
ikiwa ni kujiingiza katika ngono wakiwa na umri mdogo pamoja na biashara ya
ukahaba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...