Na afisa habari Mufindi
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi JAMHURI WILLIAM amefanya ziara katika kiwanda cha chai MTC kilichopo kijiji cha ITONA halmshauri ya Wilaya ya Mufundi baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa mwekezaji wa kiwanda hicho anakusudia kukifunga.
Mkuu wa Wilaya ameamua kufanya ziara kiwandani hapo akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya ili kufanya mazungumzo na mwekezaji huyo ajue tatizo nini mpaka afikirie kufunga kiwanda na kuhatarisha maisha ya watu wa Mufindi ambao wanaendesha maisha yao kwa kutegemea kiwanda hicho kwani kiwanda hicho pekee kimeajiri zaidi ya watu elfu 50.
Baada ya mazungumzo marefu, mwekezaji huyo alimhakikishia mkuu wa Wilaya kuwa kiwanda hicho hakitafungwa licha ya changamoto za kiuchumi anazozipitia ambazo zimesababisha tanesko wakate umeme kwa kuchelewa kulipa bili ya mwezi mmoja ya Zaidi ya shilingi milioni 100, kisha akamuomba Mkuu wa Wilaya asaidie baadhi ya changamoto zinazotokana na masuala ya kisera.
Halmshauri ya wilaya ya Mufindi inajumla ya makapuni makubwa matano (5) yaliyowekeza kwenye viwanda vya kuchakata chai kutokana na hali ya hewa rafiki kwa kilimo cha chai.
DC Jamhuri William na mmoja wa mameneja akipata maelezo ndani ya kiwanda.
Mkuu wa usalama wa taifa wa Wilaya ya Mufindi aliyevalia shati jeupe akichachangia hoja baada ya kukagua sehemu ya shehena ya mifuko mikubwa ya chai huku Mkuu wa wilaya JAMHURI WILLIAM mwenye vazi la suti nyeusi
Mkuu wa Wilaya Jamhuri William pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakitembezwa ndani ya kiwanda
Ndani ya kiwanda cha MTC na hizi ni mitambo inayotumika kuchakata chai.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Mufindi wakimsikiliza mmoja kati ya mameneja wa kiwanda hicho.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...