Na Humphrey Shao,
Globu ya Jamii.
Kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Simba Sports Club iliyokuwa ikiitwa Sunderland Arthur Mwambeta amewaomba wadau mbalimbali wa mchezo wa soka nchini na Chama cha Mapinduzi (CCM) kumsaidia kupata chombo cha usafiri kitakachomtoa sehemu moja mpaka nyingine baada ya kukatwa miguu yote miwili kutokana na maradhi yanayomkabili.
Mwambeta amesema hayo  jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na Globu ya Jamii katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam, ambako amelazwa katika jengo la Kibasila ward namba 11 baada ya kukatwa mguu Ijumaa iliyopita.

"Nimeugua maradhi haya pindi tu nilipoacha kucheza mpira hali iliyopelekea kukatwa mguu wangu wa kwanza mwaka 2015 na mwaka huu ijumaa iliyopita ndipo nilipokatwa mguu wangu wa pili na kubaki kama hivi mnavyoniona. Siwezi tena kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine kama ilivyokuwa awali...Hivyo mtu yoyote anayeweza kunisadia naomba ajitokeze " amesema Mambeta.

Amewaomba wadau kumchangia kupitia nambari hii 0714435312 ili aweze kujikwamua katika changamoto mbalimbali za kimaisha.

Pia alitoa wito kwa wapenzi na wanachama wa CCM kujitokeza kumsadia kwani wao ni moja ya watu waliokuwa wahamasishaji wakubwa kupitia TANU mpaka ilipozaliwa CCM wakitumia mpira kama sehemu ya hamasa.
 Wachezaji wa zamani wakiongozwa na Kitwana Manara wamekuwa wakimjulia hali Arthur Mwambeta ambaye amekatwa miguu yote miwili



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...