Na Rhoda Ezekiel Buhigwe,
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti amesema wameanza ziara ya siku 10 ya kutembelea na kukagua nyumba kwa nyumba ili kuwabaini watu wanaonufaika na mpango wa kuwasaidia kaya masikini TASAF awamu ya tatu, ambao hawana sifa na kuwaondoa katika Mpango.
Katika ziara hiyo iliyoanza jana katika Kijiji cha Munanila,Dc Gaguti alisema katika Wilaya ya Buhigwe kuna jumla ya kaya 307 zilizo andikishwa kama kaya masikini, lakini hazina vigezo vya kunufaika na mradi huu kutokana na hali zao za kiuchumi na mazingira wanayo ishi hayaonyeshi kuwa ni masikini hivyo watatakiwa kuondolewa katika mpango huo.
Alisema Ziara hiyo itafanyika kwa siku kumi itahusisha viongozi wote wa ngazi ya Kijiji,kata na Wilaya ili kuwabaini wale wote ambao hawastahili waondolewe na wanufaika wabaki kuwa wale wanao stahili tuu kupatiwa msaada huo wa kaya lengwa.
Gaguti alisema kuna baadhi ya wanufaika wamekimbia baada ya kupewa taarifa ya uhakiki wa wanufaika wa mradi huo kwa kuhofia wanaweza kutolewa,kwa wale ambao hawakuwepo kwenye kaya zao ili kuhakikiwa watakuwa wamejiondoa,kwa sasa tumetoa maelekezo kwa viongozi wa vijiji kushirikiana na serikali ili kukamilisha suala hilo kwa nakini bila kumpendelea wala kumuonea mtu yeyote.
"Leo tumeanza zoezi la kuwabaini wanufaika wasio na sifa zoezi,zoezi hili litakuwa ni la siku kumi katika ziara ya leo,na tumefanikiwa kuwabaini baadhi ya wanufaika ambao hawana sifa,hivyo watatakiwa kuondolewa kwenye mradi na kwa waliokwepa kufanyiwa tathimini ya kunufaika na mradi watakuwa wamejiondoa wenyewe, tunahitaji kubaki na watu ambao wana sifa ya kupatiwa fedha za TASAF ili lengo la serikali la kuzisaidia kaya masikini litimie",alisema Gaguti.

MKUU
wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti akizungumza na mmoja wa Wamufaika na mradi wa Kaya Masikini (TASAF),wakati wa ziara yake ya siku
10 ya kutembelea nyumba kwa nyumba ili kuwabaini watu wanaonufaika na
mpango wa kuwasaidia kaya masikini TASAF awamu ya tatu, ambao hawana
sifa waondolewa katika Mpango.
MKUU
wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti akiwa sambamba na Mratibu wa TASAF Wilaya ya Buhigwe Chubwa Deogratius wakiendelea na ukaguzi wa Wamufaika na mradi wa Kaya Masikini (TASAF),wakati wa ziara yake ya siku
10 ya kutembelea nyumba kwa nyumba ili kuwabaini wale watu wanaonufaika na
mpango wa kuwasaidia kaya masikini TASAF awamu ya tatu,bila kuwa na sifa katika Mpango.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...