Wajumbe
walioshiriki mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN)
anayeshughulikia masuala ya Nchi Masikini Duniani Bw. Gyan Chandra
Acharya (wa pili kulia), ambapo masuala kadhaa yakiwemo maendeleo ya
Sekta Binafsi na Miundombinu yalijadiliwa kwa kina wakati ujumbe huo
kutoka UN ulipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Ofisini kwake Jijini
Dar es salaam.

Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa kwanza kushoto),
akielezea mpango wa Serikali wa kutumia malighafi za ndani katika
kufikia maendeleo ya viwanda nchini, katika Kikao kati yake na Msaidizi
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Nchi
Masikini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (wa kwanza kulia), Mazungumzo
yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es
salaam.

Msaidizi
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Nchi
Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (kulia) akizungumza na Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) kuhusu
ushirikiano wa Tanzania na Umoja huo, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar
es salaam.

Wajumbe
walioambatana na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Nchi
Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya, wakimsikiliza Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) alipokuwa akielezea umuhimu wa
amani katika maendeleo ya Bara la Afrika, wakati wa kikao chake na
Kiongozi huyo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es
salaam.

Msaidizi
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Nchi
Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (kulia) akisikiliza kwa makini
maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb),
(hayupo pichani), alipokuwa akielezea miradi itakayowakwamua wananchi
kiuchumi ikiwemo ile ya Kilimo itakayosaidia kuendesha viwanda.
Mazungumzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango,
Jijini Dar es salaam.

Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kushoto),
akifurahia jambo wakati Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
anayehusika na masuala ya Nchi Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya
(hayupo pichani), akielezea ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na
Umoja wa Mataifa, wakati wa kikao kilichofanyika Makao makuu ya Wizara
ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...