Ng'ombe na mbuzi wakiwa wamesongamana chini ya mti pekee uliokuwepo katika eneo lililopo karibu na Shule ya sekondari ya Oljoro mkoani Arusha wakifuata kivuli ili kujikinga na jua Desemba 17, 2016. Uharibifu wa mazingira unaosabishwa na shughuli za binadamu hasa ukataji miti hovyo unaathiri hata viumbe wengine kama picha inavyoonyesha.
Mwendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda akiwa amejipumzisha katika eneo lililoathiriwa na uharibifu wa mazingira unaofanywa na binadamu katika kijiji cha Ormapinu, Arusha Desemba 17, 2016.
Wananchi wakiwa wamebeba bango lenye maneno yanayoeleza suala la uharibifu wa mazingira kuwa ni tatizo kwao katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye kijiji cha Ondenderet, Arusha Desemba 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...