Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo – TBA, Arch. Elius Mwakalinga akimkabidhi Mkataba wa Makubaliano ya mradi wa ujenzi wa nyumba 320 Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa. Hafla hiyo ya uwekaji saini makubaliano hayo ya ujenzi wa nyumba za askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Dar es Salaam imefanyika leo Desemba 19, 2016 Jijini, Dar es Salaam katika Ukumbi wa TBA. Ujenzi wa nyumba hizo ni agizo la Rais Magufuli kufuatia ziara yake hivi karibuni ambapo alitoa kiasi cha bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari wa Jeshi hilo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo – TBA, Arch. Elius Mwakalinga (kushoto) na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) kwa pamoja wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya ujenzi wa nyumba 320 za Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa TBA, leo Desemba 19, 2016 Jijini, Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo – TBA, Arch. Elius Mwakalinga na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) wakionesha nyaraka mbalimbali baada ya hafla fupi ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano ya mradi wa ujenzi wa nyumba 320 za askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Dar es Salaam.
 Maafisa Waandamizi wa Wakala wa Majengo - TBA wakifuatilia majadiliano kabla ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano ya ujenzi wa nyumba 320 za Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa TBA, leo 19 Desemba, 2016 Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia uwekaji saini wa Makubaliano ya ujenzi wa nyumba 320 za Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa TBA, leo 19 Desemba, 2016 Jijini Dar es Salaam (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...