Na Humphrey Shao,
Globu ya Jamii
MSANII na mtayarishaji wa filamu nchini ,Timoth Kachumia (TIKO) amewataja Idris Sultani na Irene Paul kuwa watasindikiza usiku wa wa kachumbari utakaofanyika katika ukumbi wa Aqua Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Globu ya Jamii Tiko amesema kuwa wasanii hao pia watapata fursa ya kuonyesha filamu yao kwa mara ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘Kiumeni’.
“Kachumbari show" itajumuisha vitu vingi sana ambapo wasanii tofauti watakapowekwa katika jukwaa moja na kufanya kazi tofauti za sanaa ikiwemo sanaa za maonyesho za majukwaani muziki wa bongofleva na filamu”amesema Tiko.
Ameweka wazi kuwa katika shoo hiyo kutakuwa na mashindano ya kutafuta vipaji na Stand Up Comedy kutoka kwa wasanii wakali katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...