Kampuni ya JUNACO Group of Companies mwishoni mwa wiki ilizindua kifaa cha kisasa kinachotumika kuzima moto kwenye makazi ya watu na mitambo kinachofahamika kama ‘FirePro’ ikiwa ni uvumbuzi unaolenga kukabiliana na janga hilo hatari.

Akizungumza wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa kifaa hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambao ya Ndani Balozi Hassani Simba Yahya, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo hapa nchini , Bw Justine Lambert alisema matumizi ya kifaa hicho miongoni mwa watanzania yatasaidia kuondoa athari za uharibifu wa mali na vifo vitokanavyo na majanga ya moto kwenye makazi ya watu.

“Uvumbuzi na ujio wa kifaa hiki ni ishara kwamba athari zitokanazo na majanga ya moto ambayo yamekuwa yakiripotiwa kupoteza maisha ya watanzania na kusababisha umasikini kutoka na uharibifu wa mali sasa linakwenda kwisha,’’ alisema Bw Lambert huku akiongeza kuwa wao kama sekta binafsi wana wajibu wa kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi wake.

Alisema mbali na suala la kuhakikisha usalama wa watanzania, uwepo wa kifaa hicho pia utaongeza ajira kwa wadau wote watakaohusika kwa namna moja au nyingine katika mauzo ya kifaa hicho hapa nchini.“ Ndani ya miaka minne ijayo Junaco Group of Companies tunarajia kutengeneza ajira zipatazo 780 zitakazohusisha wauzaji, wasambazaji na wataalamu wa kufunga kifaa hiki kote nchini,’’ alisema.
2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimsikiliza George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa akitoa maelezo ya jinsi vifaa hivyo vinavyoweza kuzima moto katika mitambo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam, wa pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies na wa tatu ni Fikili S. Salla Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya moto Jeshi la Zimamoto.
3
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimsikiliza George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa akitoa maelezo ya jinsi vifaa hivyo vinavyoweza kuzima moto katika mitambo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam, wa pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies.
1
George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus akionyesha moja ya kifaa cha kuzima moto kinachoweza kufungwa katika mitambo mbalimbali chenye uwezo wa kuzima moto katika hatua za awali kabisa kabla ya kuwa mkubwa wakati alipokuwa akielezea ubora wa vifaa hivyo katika kupambana na majanga ya moto kwenye uzinduzi ulifanyika Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam mwishono mwa wiki.

7
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kifaa hicho cha Firepro mwishoni mwa wiki.
5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimpongeza George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus mara baada ya kumaliza kutoa maelezo yake mbele ya wageni waalikwa wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam, katikati ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...