Kampuni ya kizalendo ya Grand Tech  imejitolea kujenga barabara ya Kurasini Shimo la Udongo jijini Dar es salaam kwa kiwango cha zege kwa urefu wa Kilomita moja, kama sehemu ya kurudisha ilichokipata kwa jamii na kuunga jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Rais John Pombe Magufuli.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni hiyo inajihusisha na ujenzi wa barabara na makazi,  Bw. Atu Patrick Mwakitwange,  amesema kuwa wameamua kuunga mkono jitihada za serikali kwani eneo hilo la Shimo la Udongo ambalo lilitengwa na serikali kwa ajili shughuli za bandari ili kuinua uchumi wa nchi ni eneo muhimu sana kwa jiji. 
"Baada ya kukubali kutengeneza mita 500 Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa alituomba tumalizie mita 500 zilizosalia ili kukamilisha kilomita moja nasi hatukumkatalia", aliseme Bw. Mwakitwange.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amesema kuwa Dar es Salaam inajengwa na wana Dar es Salaam wenyewe hivyo kila mmoja kwa mchango kusaidia kadri awezavyo kama walivyojitokeza wazawa na Grand Tech kujenga barabara hiyo huku akiongeza kuwa hao ndiyo wazawa wa kwanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam kujenga barabara na kuwaomba wadau wengine waige mfano huo. 
"Barabara hii ina tija kubwa kwa serikali kwani ujenzi wake kwa kiwango cha zege utasaidia malori kupita bila kufanya uharibifu kama ilivyokuwa awali, pia ujenzi huo utasaidia kupunguza foleni kuelekea eneo la Bandari", alisema RC Makonda.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akiwa na watendaji wa Kampuni ya kizalendo ya Grand Tech  na wananchi akikagua barabara hiyo.


Kampuni ya kizalendo ya Grand Tech akizindua ujenzi wa barabara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...