Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media,
kampuni inayomiliki mtandao maarufu, Jamii Forums, Maxence Melo.
Maxence Melo ambaye ni mwanzilishi wa Jamii Forums, anashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam (Central Police) toka jana na leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyoko Mtaa wa Lumumba kwa madai kuwa amekataa amri ya jeshi la polisi kutoa taarifa za siri za watumiaji wa mtandao huo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye mtandao huo, Max amenyimwa dhamana.
“Maxence Melo amekamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari,” umeandika mtandao huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...