Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema atabadilisha uongozi wa menejimenti ya kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), kwa kushindwa kutekeleza uendeshaji na usimamizi wa kampuni hiyo.

Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo na kuonesha kutoridhishwa na huduma zinazotolewa na MSCL, Prof. Mbarawa amesema kutokana na kampuni kushindwa kujiendesha kibiashara na kulipa mishahara kwa wafanyakazi wake amelazimika kuchukua maamuzi hayo ili kuinusuru kampuni hiyo.

“Sijaridhishwa na taarifa za mahesabu yenu katika uendeshaji wa huduma za meli katika ukanda wa Ziwa Viktoria, Hamuwezi kusafirisha mizigo milioni 3.6 na nyie mkapata faida ya laki 2.. hamuomyeshi umakini kwenye utendaji”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha, katika kuhakikisha huduma za Kampuni hiyo zinaimarika Serikali kupitia Waziri huyo imeahidi  kutoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukabarati wa meli nne zilizokuwa zimekufa katika ukanda huo ili kuboresha huduma za usafiri wa Ziwa.

Prof. Mbarawa amezitaja meli zitakazokarabatiwa ni Mv. Clarious, Mv Serengeti, Mv Sangara na Mv. Ukerewe ambazo zinahitaji ukarabati wa injini, mifumo ya umeme na ufundi na gia boksi.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), wakati alipotembelea ofisi hizo mkoani Mwanza.
 Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), Bw. Erick Hamis akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu hali ya utendaji wa kampuni hiyo katika ukanda wa Ziwa Viktoria, mkoani Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  John Mongella, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na menejimenti na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), wakati wa ziara ya Waziri huyo katika ofisi hizo mkoani Mwanza.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  John Mongella, wakati alipotembelea ofisi za Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), mkoani Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...